Subscribe Now
Sign up for our newsletter to receive the latest updates.
Mbinu Yetu Kuu
Ili kufikia malengo haya, tunasaidia katika kuendeleza umoja imara na wenye shughuli wa wakazi wa mijini wenye kipato cha chini. Msaada huu unajumuisha kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa; uhamasishaji na uandishi wa rasilimali za jamii; kufanya uhesabuji na upangaji ramani; ziara za kujifunza; usaidizi wa ushirikiano, msaada wa kiufundi, kujenga uwezo, uongozi na usimamizi, uhamasishaji, utetezi, tafiti zenye mwelekeo wa vitendo na uthibitishaji wa taarifa.
Dhamira ya CCI ni kujenga uwezo wa jamii kutoka kwenye maeneo duni ya mijini kuanzisha maendeleo endelevu yatakayoboreshA maisha yao.
CCI inalenga kujenga miji yenye usawa na jumuishi ambako jamii kutoka maeneo duni zitakuwa na umoja, zitapewa uwezo na stadi muhimu ili kujadiliana kwa ufanisi kuhusu masilahi na vipaumbele vyao vya pamoja.
Centre for Community Initiatives (CCI) ni shirika lenye ajenda ya kupambana na umasikini wa mijini, likifanya kazi na kuandaa jamii zinazoishi katika makazi holela katika miji 8 nchini Tanzania. Miji hiyo ni Dar es Salaam katika Halmashauri zote, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mara, Arusha, Tanga na Zanzibar. Upanuzi wa programu za kusaidia wakazi wa maeneo duni unaendelea kulingana na mahitaji na rasilimali zilizopo.
Hasa Tanzania ina kiwango cha tatu kwa kasi ya ukuaji wa maeneo duni barani Afrika, zaidi ya 6% kwa mwaka, na idadi ya sita kwa ukubwa wa wakazi wa maeneo duni, zaidi ya watu milioni 6 wanaoishi katika maeneo hayo. Wametengwa na maisha na fursa za miji rasmi, hivyo wakazi wa maeneo duni mara nyingi hawajulikani katika ajenda nyingi za maendeleo ya mijini na hatimaye wengi kuishi katika mazingira duni bila kumiliki ardhi, nyumba duni, vitisho vya kufukuzwa, ukosefu wa maji na usafi wa mazingira. Kwa muda mrefu, wakazi wa mabanda wamekuwa wakitarajia mamlaka za Serikali kuingilia kati kutatua changamoto zao bila mafanikio.
CCI inafanya kazi na wakazi wa maeneo duni kwa dhumuni kuu la kuwawezesha jamii kubuni mbinu mpya za kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha mahitaji na madai yao yanashughulikiwa. Wakazi wa maeneo duni wanapaswa kuweka kipaumbele kwenye mahitaji yao na kueleza matarajio yao ili wawe wadau muhimu katika kubadilisha miji kwa kubaini mahitaji yao na kupanga suluhisho nafuu na linalowezekana.