CCI inaunga mkono jamii kujiandaa kupitia mtandao wa vikundi vya kuweka akiba vinavyojulikana kama Tanzania Federation for Urban Poor (TFUP). Uundaji wa jamii unalenga kuleta ushirikiano wa pamoja katika kukabiliana na changamoto za makazi holela, ambazo mara nyingi haziwezi kutatuliwa kwa kiwango cha mtu mmoja mmoja.
Zaidi ya hayo, unalenga kutoa sauti kwa vipaumbele vya jamii mbele ya Mamlaka husika kama vile Serikali za Mitaa na taasisi za huduma. Jamii inapokuja pamoja, huwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuelewa, kutambua changamoto, kubuni mawazo ya ufumbuzi, na kwa pamoja kutekeleza mipango iliyowekwa.
Mtandao wa Tanzania Urban Poor Federation haufanyi kazi kwa manufaa ya wanachama pekee, bali pia kama kichocheo cha kuhamasisha jamii kubwa zaidi kuchukua hatua. Kwa sasa, Shirikisho linafanya kazi katika miji 8 ya Tanzania ambayo ni Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mara, Arusha, Tanga na Zanzibar na lina wanachama 17,000.