Mfuko wa Maskini wa Mijini Tanzania (JENGA) ni utaratibu wa maendeleo ya kifedha ulioanzishwa mwaka 2008 na Shirikisho la Tanzania kwa ushirikiano na CCI. Ni utaratibu unaowezesha mashirika maskini mijini kupata fedha kwa kujenga uwezo wao wenyewe.
Madhumuni ya mfuko huo ni kutoa chanzo cha mtaji nafuu kwa idadi inayoongezeka ya mifuko ya akiba wanaoishi katika makazi holela kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaisha na maendeleo ambazo haziwezi kufikiwa na taasisi za fedha za jadi.
Mfuko wa Maskini wa Mijini Tanzania (JENGA) unatoa mikopo nafuu kwa ajili ya manunuzi ya ardhi; ujenzi wa nyumba na uboreshaji; shughuli za kuongeza kipato; maendeleo ya miundombinu kama vile maji, usafi wa mazingira (ujenzi wa vyoo, vifaa vya kumwaga mashimo, vyoo vya umma, na udhibiti wa taka ngumu). Chanzo cha mtaji wa fedha hizo ni kutoka kwa akiba ya jamii pamoja na ruzuku/ mikopo yenye masharti nafuu kutoka kwa wafadhili.