Warsha ya mwisho ya wadau ya ACRC UPTAKE jijini Dar es Salaam ilifanyika tarehe 31 Machi, 2023 kwa ajili ya kuwasilisha matokeo muhimu na Changamoto Shirikishi za Kipaumbele (PCP’s) zilizobainishwa katika utafiti kutoka sekta au maeneo mbalimbali.
Lengo la warsha hiyo lilikuwa kuboresha matokeo ya utafiti pamoja na PCP’s. Mgeni rasmi aliyemwakilisha Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bi. Catherine Pye, alishiriki katika warsha hiyo. Pia alikuwepo mwakilishi wa ACRC kutoka Nairobi, Kenya kupitia taasisi ya Partnership for African Social and Governance Research, Bw. Martin Atela, pamoja na wadau muhimu ambao ni watunga sera serikalini wakiwemo Meya wa Halmashauri ya Temeke Mhe. Abdallah Mtinika, madiwani, watafiti kutoka vyuo vikuu, viongozi wa jamii kutoka Kata na mitaa, vikundi vya wajasiriamali kama VIBINDO, vikundi vya Shirikisho la Maskini wa Mjini (Urban Poor Federation), vyama vya ushirika wa makazi, na wawakilishi wa asasi zisizo za kiserikali kama Haki Ardhi, Habitat for Humanity na Frederick Engelbert Stiftung.
Utafiti huu ulichunguza sekta kuu au maeneo (domains) mbalimbali kama vile sekta ya makazi, sekta ya makazi holela, maendeleo ya kiuchumi ya mitaa na kata, mageuzi ya kiuchumi (structural transformation), mfumo wa jiji (city of systems) na mipangilio ya kisiasa (political settlement).
Kwa mwisho, watafiti walipata fursa ya kutafakari pamoja na wadau kuhusu suluhisho la Changamoto Shirikishi za Kipaumbele (PCP’s), na watafiti hao waliweka ahadi ya kuyaboresha na kuyahuisha PCP’s zao kabla ya warsha inayofuata na hatua nyingine za utekelezaji wa utafiti.
Add New Comment