CCI kwa kushirikiana na Chuo cha Ardhi (Ardhi University) waliratibu warsha kuhusu Kikoa cha Makazi (Housing Domain).
Madhihirisho ya matokeo muhimu yaliyopatikana kutoka katika makazi mbalimbali ya utafiti katika Jiji la Dar es Salaam yaliwasilishwa na Dkt. Tatu na Profesa Kyessi kutoka Chuo cha Ardhi.
Washiriki walioalikwa kutoka sekta za Makazi na Ardhi wakiwemo asasi za kiraia kama Haki Ardhi, Taasisi za mikopo midogo ya makazi, watafiti, maafisa wa mipango miji na ardhi kutoka halmashauri, pamoja na viongozi wa Kata na Mitaa, walipata fursa ya kutoa maoni na kuongeza uelewa zaidi ili kuboresha matokeo hayo na kuangazia masuala na changamoto zinazohusiana na Kikoa kingine kama vile Mfumo wa Jiji (City of Systems), Makazi Holela (Informal Settlements) na Mipangilio ya Kisiasa (Political Settlements).Baadhi ya matokeo muhimu ya Kikoa cha Makazi (Housing Domain) ni pamoja na:
- Uwezo mdogo wa wananchi wengi wa kipato cha chini kumudu kujenga au kumiliki nyumba.
- Uwepo wa Sera ya Maendeleo ya Makazi ya kale ambayo haina msingi madhubuti katika kuendeleza Sekta ya Makazi.
- Changamoto ya wananchi wengi kutotumia wataalam katika ujenzi wa nyumba zao.
Kwa hitimisho, washiriki wa warsha walikubaliana kuunda Jukwaa la Sekta ya Makazi (Housing Sector Forum) ambalo litaongoza na kushughulikia changamoto za sekta hiyo. Awali, jukwaa hilo litaratibiwa na Center for Community Initiatives (CCI) kama sekretarieti ya jukwaa.
- Uwezo mdogo wa wananchi wengi wa kipato cha chini kumudu kujenga au kumiliki nyumba.
2023-09-01
Add New Comment