CCI kwa kushirikiana na Chuo cha Ardhi (Ardhi University) ilikaribisha walimu na wanafunzi kutoka University College London wanaosoma Shahada ya Uzamili (Masters) katika Mazingira na Maendeleo Endelevu kwa kipindi cha wiki mbili katika Jiji la Mwanza. Wanafunzi waliogawanyika katika makundi mbalimbali walijifunza kwa vitendo kuhusu mifumo ya umiliki wa ardhi iliyopo katika makazi holela ya Kambarage na kuchunguza kwa kina masuala ya jinsia, kanuni za kijamii, kanuni ndogo (by-laws) na mila zinazohusiana na masuala ya usafi wa mazingira katika eneo la Kigoto.

Zaidi ya hayo, wanafunzi walipata fursa ya kushirikiana na Vikundi vya Shirikisho la Maskini wa Mjini Tanzania (Tanzania Urban Poor Federation) jijini Mwanza. Walikusanya taarifa kuhusu ushirikiano wa kifedha wa wananchi wa msingi (grassroots co-financing) kwa ajili ya kuboresha usafi wa mazingira na kuelewa jinsi Mwanza City Sanitation Forum na Mfuko wake ulioanzishwa hivi karibuni unavyoweza kuwa na faida kwa wakazi wengi wanaoishi katika makazi holela kama Mabatini kupitia mikopo ya usafi na ruzuku.

Kwa upande mwingine, wanafunzi walichunguza mfumo rahisi wa maji taka (simplified sewerage system) na mchakato wa closing the loop ili kuelewa mnyororo wa thamani wa usafi wa mazingira na hatua za mwisho za mnyororo huo. Kwa ujumla, uzoefu wa kujifunza na utafiti wa kisayansi uliofanywa utashirikiana na uchapishaji wa waraka wa sera (policy briefs) ambao utatafsiriwa kwa Kiswahili ili kufikia hadhira kubwa zaidi jijini Mwanza na nchini Tanzania kwa ujumla.