Shirikisho linahamasisha usafi kupitia utoaji wa elimu kutoka kaya hadi kaya na kupitia mikutano ya jamii. Timu za usafi na udhibiti wa taka ngumu hupewa mafunzo na CCI kwa ajili ya kuhamasisha usafi na ukusanyaji wa taka ngumu ndani ya makazi yao kwa kushirikiana na mamlaka husika. Baadhi ya vikundi hivi vimetambuliwa rasmi na sasa vina uwezo wa kushindania zabuni kutoka kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hivi karibuni, shirikisho limeanzisha na kuunganisha shughuli za ukusanyaji wa taka ngumu na urejelezaji (recycling) ili kuongeza thamani ya taka katika kuzalisha mbolea na bidhaa nyingine, hivyo kuongeza kipato kwa vikundi. Hatua hii pia itapunguza gharama za kusafirisha taka hadi kwenye madampo ambayo mara nyingi yako mbali au nje ya jiji. Kama sehemu ya kuanzia, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetenga eneo la bure la ukubwa wa mita mraba 3,200 kwa ajili ya shirikisho na CCI kufanya kazi za urejelezaji.
Add New Comment