Mradi wa uzalishaji wa nishati ya gesiasilia itokanayo na kinyesi chabinadamu ulibuniwa na kujengwa nashirika la Centre for Comm unityInitiatives, CCI kwa kushirikiana naVikundi vya kijamii (Federation), katika mtaa wa Mji Mpya kata ya VingungutiWilaya ya Ilala, Dar es S alaam . Mpangohuu ambao ulibuniwa mwaka 2020 unalenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, katika jamii ya wakazi waishio katika makazi holela pamoja na kutatua changamoto ya masuala muhimu ya usafi wa mazingirana uboreshaji wa vyoo. Kutokana nauhalisia wa eneo la vingunguti kujaa maji mengi na kushindwa kuchimba mashimo makubwa ya vyoo nakusababisha kinyesi kutapakaa katika makazi ya watu na kusababisha milipuko ya magonjwa wakati wa mvuakubwa.
Mradi huu wa uzalishaji wa gesi una lengo la kuwezesha upatikanaji wa gesi asilia inayotokana na kinyesi cha binadamu kutoka kwenye vyoo vilivyoboreshwa.
Mradi huu ulihusisha uboreshaji wa vyoo nakuunganisha vyoo 10 katika mfumo wa B iogasi,utandazaji wa bomba za kusafirishia k inyesi naujenzi wa mtambo ambapo kinyesi hukusanywana kuanza kuzalisha gesi. Mabomba maalumu yanawekwa ili kusafirisha gesi hiyoinayozalishwa hadi kwenye kaya kama nishatikwa matumizi ya kupikia. Kwa sasa vnyoo 20 vimeunganishwa katika mfumo huo wenyeuwezo wa 10m³. Kutokana na mafanikio hayo CCI ilibuni mradi mwingine wa mtambo wakuzalisha gesi itokanayo na kinyesi katika mtaajirani wenye uwezo wa 20m³ Na unauwezo wakuunganisha vyoo 50 ambapo ni mara mbili ya uwezo wa mradi wa awali.
Gharama za mradi huu zilihusisha uboreshaji wa vyoo ili kila kaya iweze kuunganishwa na mfumo wa uzalishaji wa gesi itokanayona kinyesi, ambapo shirika la CCI liligharamia gharama za mabomba pamoja na gharama za uchimbaji wa m tam bo wakuzalishia gesi. Vikundi vya Federation vilihamasisha jamii kushiriki katika mradi na kuunda vikundi vya Federation katika maeneo hayo. Wanajamii waliohamashishwa walishiriki kwakutoa maeneo yao kupitisha mabomba na kuchangia nguvu kazi wakati wa uchimbaji wa mitaro ya kupitisha mabomba.
Mnufaika katika mradi:
“ Naushukuru sana mradi huu kwa kuwezakutufikia sisi watu wa kipato cha chini,kwani tunatakiwa kutafuta mifumo yanamna hii kuangalia gharama za maisha yakila siku. Nyumbani kwangu nilitumia pesanyingi kununua nishati ya kupikianyumbani. Kwa mwezi mmoja nilikuwanikitumia zaidi ya shiling 75,000 Tshambayo kwa Maisha yangu ni kubwa sanana inaweza kutumika kwa matumizimengine kama vile matibabu na kununuachakula kama inavyotumika sasa maraninapoanza kutumia gesi. Ningependa nakushauri miradi ya namna hii ipewekipaumbele na ijengwe katika maeneo yawatu wa kipato cha chini ili ipunguzeongezeko la gharama za maisha katikakaya zao. Kwa sasa napika milo yotekuanzia asubuhi hadi jioni na ninapikavyakula vya kila aina kupitia nishati hiiinayotokana na kinyesi cha binadamu”.Sakina Gumbo (Mnufaika wa gesi asiliaitokanayo na kinyesi)
Shirika la CCI bado linaendelea na utafitiwa jinsi ya kusambaza gesi asilia itokanayo na kinyesi cha binadamu ili watu wengi Zaidi waweze kunufaika. Aidha shirika la CCI linaunga juhudi zinazofanywa na Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais waJamuhuri ya Muungano wa Tanzaniakatika kujenga na kubuni miradi ya nishatimbadala ambayo inasaidia kupunguza gharama za matumizi ya mkaa, pamoja naumeme. Ubunifu uliofanywa na CCI umeonesha umuhimu wa rasilimali yakinyesi ambayo huonekana kutokuwa nathamani katika kuzalisha gesi asiliaambapo CCI imeweza kutatua changamoto ya gharama za manunuzi ya gesi, umeme na mkaa kwani upatikanaji wa gesi hii asilia haigharimu matumizi ya pesa ili kununua nishati.